HabariNews

Vinara wa ODM Waanzisha Ziara ya Usajili wa Wanachama  Pwani

Kiongozi wa Chama cha ODM Odinga  ameanza ziara yake katika kisiwa cha Manda na Kisiwa cha Lamu katika kile ambacho kimetajwa kama njia ya kupigania nafasi ya kisiasa eneo hilo lililotengwa kihistoria.

Akiungwa mkono na Gavana wa Mombasa Abdullswamad Sherrif Nassir ambaye aliongoza wajumbe wa chama hicho na kuweka wazi mjadala wa hivi majuzi wa kisiasa kuhusu mustakabali wa Azimio.

Gavana Nasir aliandamana na wambunge wa Mombasa akiwemo Mwakilishi wa Wanawake wa Mombasa Zamzam Mohamed, mbunge wa Likoni Mishi Mboko , mbunge wa jomvu Bady Twalib
pamoja na Spika wa Bunge la Kaunti ya Mombasa Aharub Khatri.

Ni dhahiri kuwa Gavana Nassir atakuwa na jukumu kubwa kisiasa huku wanasiasa wengi wakionekana kuungana Pwani katika miezi ya hivi majuzi.

Hata hivyo mikutano zaidi iliyoratibiwa katika kaunti za Tana River, Kilifi, Taita Taveta na Kwale ambayo itafikia kilele cha mkutano mkubwa huko Mombasa siku ya Jumamosi.

Haya yanajiri siku chache  tu baada ya kuongoza kundi la viongozi wa Pwani kwenye ukumbusho wa aliyekuwa Makamu wa Rais marehemu Jaramogi Oginga Odinga mjini Kisumu.

BY NEWS DESK