HabariNews

Magavana Walilia Serikali Kuu!

Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Magavana Ahmed Abdullahi ameikosoa Wizara ya Fedha na Hazina ya Kitaifa kwa kucheleweshwa kwa utoaji wa fedha kwa serikali za kaunti.

Kulingana na Abdillahi, ukame wa rasilimali kwa kaunti umekuwa desturi na mtindo wa kila mwaka suala ambalo limelemaza malengo ya ugatuzi kama inavyokusudiwa na Katiba ya mwaka 2010.

Abillahi ambaye pia ni Gavana wa Wajir amebaini kuwa Wizara hiyoya fedha imekuwa ikipuuza Idara ya Mgao wa Mapato ya Kaunti (CRA) na Baraza la Mgavana, CoG.

Magavana aidha wamelalamikia kuwa kucheleweshwa kwa mgao huo wa fedha kumeathiri vibaya utoaji wa huduma huku mwenyekiti wa Baraza la Magavana Anne Waiguru akisema kaunti hazijalipa mishahara tangu mwezi Novemba mwaka jana.

Waiguru amefichua kuwa baadhi ya kaunti nyingine zinmelazimika kutafuta fedha za ziada ili kuwakimu na kushughulikia matakwa ya wafanyakazi wao.

Inasemekana kuwa kufikia tarehe 19 Januari mwaka huu Hazina ya fedha ilikuwa haijatoa shilingi bilioni 81 inazodaiwa na kaunti.

BY NEWSDESK