HabariNews

Kenya Power yatangaza umeme kukatizwa katika maeneo mbalimbali nchini hii leo

Shirika la usambazaji umeme nchini Kenya Power limetangaza kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo mbalimbali nchini hii leo.

Katika taarifa waliotoa kupitia mtandao wao wa X (zamani Twitter) shirika hilo limetangaza baadhi ya maeneo ya kaunti 6 nchini  yatakosa umeme kuanzia mwendo wa saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.

Kaunti hizo ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa nguvu za umeme ni pamoja na kaunti za Mombasa, Kilifi, Taita Taveta, Nairobi, Elgeyo Marakwet na Nyeri.

Katika kauti ya Mombasa maeneo yatakayoathirika ni eneo la Changamwe, Migadini, katika Hospitali ya Port Reitz, Chaani, laini ya pili ya SGR na maeneo yaliyo karibu.

Huko kaunti ya Kilifi sehemu kadhaa za maeneo ya Kikambala, Kanamai, Barani, Four Farm, Kwa Mwamweni, Mavueni, Chasimba, Mwarakaya, Dzitsoni na Jaribuni zinakosa umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.

Vile vile Kaunti ya Taita Taveta maeneo ya Miasenyi, Wangala, Misharinyi na sehemu zilizopakana ni miongoni mwa maeneo yaliyoathirika na kupotea kwa umeme.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Gigiri na Muthaiga zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

BY NEWS DESK