HabariLifestyleMombasaNews

Afueni Kwa Kina Mama Wajawazito Wadi Ya Chaani

Ni afueni kwa kina mama wajawazito kutoka wadi ya Chaani kaunti ya Mombasa baada ya mwakilishi wadi eneo hilo Franklin Makanga kuzindua mradi wa kuwasaidia kina katikaa safari yao ya kubeba Mimba.

Akizungumza katika uzinduzi huo mnamo Alhamisi 14 Makanga amesema mradi huo unalenga kuwapunguzia gharama ya matibabu katika kipindi hicho pamoja na kupunguza visa vya kina mama kupoteza maisha wakati wa kujifungua akiongeza kuwa Kungali na takwimu za juu za vifo vya kina mama wakati wa kujifungua.

Aidha Makanga alisema ni hatua moja inayopiga jeki mpango wa afya mashinani huku akiwahimiza kina mama hao kutembelea hospitali za kiserikali ili kurahisisha mradi huo.

“Hili ni zoezi amabali tunalifanya tukiwa tunakusudia kina mama gharama ya kubeba mimba pili itapunguza magonjwa na maradhi ambayo hutokea kipindi hicho tatu itatusaidia afya za kina mama katika juhudi za kuhakikisha kina mama wanajifungua watoto afya nzuri.” Alisema Makanga

Kwa upande wake Susan Wanjohi ambaye ni afisa wa nyanjani alisema mradi huo utarahisisha kazi yao kutokana na kutambua kina mama wajawazito akidokeza kuwa mara nyingi kina mama wanapitia changamoto za kufika hospitali.

“Kina mama wengi wanapitia changamoto nyingi hawana chakula,kwenda hospitali ni gharama ningependa kumshukuru kwa kuungana na madkatari wa nyanjani ametushika mkono na ameturahisishia kazi kwa sababu kutambua kina mama wajawazito.” Alisema Susan

Nao kina mama watakaonufaika na mradi huo walimpongeza mwakilishi wadi huyo kwa kuanzisha mradi huo wakisema itawasaidia pakubwa hasa wale ambao wanakumbwa na hali duni ya maisha.

“Ningependa kumpongeza mweshimiwa kwa mradi huu manake kuna wengine ambao hatuna chochote na nina imani mradi huu utatusaidia,hali zetu ni duni na hatujiwezi “ Walisema Kina mama.

BY MEDZA MDOE.