NewsSiasa

Jumla ya kaunti 38 zimepitisha mswada unaolenga kubadilisha katiba wa BBI kufikia sasa.

Kaunti 27 zimepigia kura mswada huo hii leo huku mabunge ya kaunti ya Kwale, Tana River, Embu ,Isiolo, zikiwa kaunti za hivi  punde kupitisha mswada huo wa BBI.

kaunti ya Mombasa,Taita taveta , migori miongoni mwa kaunti zengine ,zilizopitisha mswada huo wa BBI bila ya kupingwa.

Katika kaunti ya Kwale wawakilishi wadi 34 waliohudhuria mkao ,wakiongozwa na  kiongozi wa wengi,James Dawa,Hanifa Mwajirani na  Raiaa Mkungu ,wanasema kuwa marekebisho ya katiba kupitia BBI itasaidia pakubwa kaunti ya Kwale, hususan katika masuala ya uakilishi katika bunge la kitaifa pamoja na kuongezwa kwa mgao wa serikali za kaunti.

Kaunti ya Kwale ikiwa na matarajio ya kupata maeneo bunge mapya 3 iwapo BBI itapita katika kura ya maamuzi .

 

Kwa upande wao kule kaunti ya Lamu ,wakiongozwa na  kiongozi wa wengi katika bunge la Lamu  Abdallah Aboud maarufu Baabad, wanasema kuwa wameipitisha BBI kwa kuwa itaboresha zaidi ugatuzi kwa kuwapa hazina ya maendeleo ya maeneo wadi.

 

Katika eneo la Bonde la ufa linalokisiwa kuwa eneo lenye ufuasi wa naibu wa rasi William Ruto,kaunti zote zimepitisha mswada huo kufikia sasa ipokuwa kaunti ya Baringo ambayo ndio kaunti pekee iliyopinga mswada huo.

Hatahivyo kaunti zote zilizopiga kuwa kutoka maeneo za magharibi ,Maharikiri, Nyanza , Kazkazini, Mashariki na Pwani zimepitisha mswada huo.

Ikumbukwe idadi ya mabunge 24 ndio inahitajika kupitisha mswada huo.

Kufikia sasa Kaunti 8 bado hazijapigia mswada wa BBI kura

Ni wazi sasa wakenya wataelekea kwenye kura ya maamuzi kufuatia uamuzi huo wa mabunge ya kaunti.