Waziri wa elimu Pro George Magoha leo anafanya ziara katika mitaa ya mabanda eneo la Jomvu na Changamwe kuwatembelea wanafunzi ambao watanufaika na msaada wa elimu kutoka kwa mpango wa ufadhili wa elimu.
Wanafunzi 9,000 kote nchini watanufaika na mpango huo, 62 wakitoka katika mtaa wa Bangladesh hapa Mombasa.
Aidha Magoha amesema kuwa wanafunzi wote watakaonufaika na mpango huo wa serikali watapelekwa katika shule za mabweni ili kuwapa wakati mwema wa kujiendeleza kimasomo.
By Reporter