Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi amewaonya wakaazi kaunti ndogo ya Malindi kukoma kuuza mashamba kiholela.
Akizungunza kwenye halfa ya kutoa vyeti takriban 800 vya umiliki wa ardhi mjini malindi Kingi amewataka wenyeji hao kujivunia makao yao wakiwa wamiliki halali.
Kingi ameitaka serikali kuu kuendelea kusambaza miradi ya maendeleo kaunti hiyo akisema wakaazi bado wako na mahitaji zaidi.
Wakati uohuo wenyeji walionufaika na ugavi huo wa hati miliki wameelezea furaha yao na kuahidi kutumia vyeti hivyo kwa manufaa yao.
Wameapa kutouza ardhi zao badala yake wameashiria kupeleka hati hizo kwa benki mbali mbali ili waweze kupata mikopo endapo watakumbwa na changamoto zozote.
Juma hili Rais Uhuru Kenyatta alizindua shuhuli hiyo ya ugavi wa hati miliki kaunti ya Kilifi huku zaidi ya wenyeji 3,000 wakitarajiwa kunufaika na zoezi hilo.
By News Desk