Kinara wa chama cha ANC musalia Mudavadi amekashifu serikali kwa kutumia njia zisizofaa katika kuongeza pesa za kulipa madeni.
Mudavadi amesema njia zinazotumiwa na serikali kutafuta pesa kulipa madeni zinaathiri wananchi wa kawaida akipigia mfano kama kuongeza bei ya mafuta na kawi .
Aidha amesema badala yake serikali inapaswa kufanya makubaliano ya kuhairisha tarehe za kulipa madeni.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kituo kimoja cha radio na kuongeza kuwa serikali inafaa kusimamisha baadhi ya miradi inayoendelea na kutumia fedha hizo katika kuimarisha uchumi .
Haya yanajiri baada ya bei ya mafuta na kawi kupanda sana katika historia ya kenya huku wananchi wakihofia kupanda kwa bei za nauli na bidhaa zengine.
BY NEWS DESK