Serikali ya Kitaifa imezindua rasmi mpango wa ugavi wa chakula cha msaada kwa waathiriwa wa baa la njaa katika eneo la Pwani.
Akizungumza kwenye eneo la Chakama katika Kaunti ya Kilifi, Waziri wa Ulinzi humu Nchini Eugene Wamalwa amesema kwamba Serikali imetenga kima cha takriban shilingi bilioni 2 kukabiliana na makali ya ukame humu Nchini.
Wamalwa aidha ameutaja ukosefu wa mvua katika msimu unaotarajiwa, kusababisha ukame unaendelea kushuhudiwa.
Ugavi wa chakula unatekelezwa kwa kipindi cha wiki mbili zijazo na haya yanajiri wakati ambapo zaidi ya watu laki tatu, elfu sabini na tano na mia tisa kwenye eneo la Pwani wakikumbwa na ukosefu wa Chakula.
BY NEWS DESK