Baadhi ya vituo vya usajili katika maeneo ya Lamu Magharibi havijasajili hata mtu mmoja.
Hali hii inatajwa kuchochewa na visa vya utovu wa usalama ambavyo viliripotiwa kwenye eneo hilo siku za hivi karibuni huku visa hivyo vikisababisha baadhi ya wakaazi kupoteza vitambulisho vyao vya Kitaifa.
Maeneo hayo ni Mikinduni, Nyatha, Juhudi, Mavuno, Witu, Holy Angels, Hindi na Poromoko.
Meneja wa Tume ya Uchaguzi ya IEBC Tawi la Lamu Mohammed Adan, amesema kwamba licha ya vifaa vya usajili kusambazwa kwenye vituo vyote vya maeneo hayo hakuna yeyote ambaye amejitokeza kusajiliwa.
Wakati uo huo Adan anahisi kwamba huenda Kaunti hiyo ikakosa kufikia idadi ya wapiga kura waliolengwa kusajiliwa kwenye awamu hii.
Itakumbukwa kwamba awamu hii ya pili iliyoratibiwa kufanyika kwa siku 30, ilianza kung’ao nanga rasmi siku ya Jumatatu wiki hii.