AfyaHabariNews

Kijiji cha Mpirani katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi kimeshangaza wahudumu wa afya pamoja na viongozi katika wizara ya afya kutokana na idadi kubwa ya watu wanaoishi na ulemavu.

Kijiji cha Mpirani katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi kimeshangaza wahudumu wa afya pamoja na viongozi katika wizara ya afya kutokana na idadi kubwa ya watu wanaoishi na ulemavu.
Watu 250 kati ya 500 kutoka eneo bunge hilo wanaishi na ulemavu wote wakipatakina katika kijiji cha Mpirani.Wakaazi sasa wanaitaka serikali kuu kutuma watafiti wa masuala ya afya ili kubaini chanzo cha ulemavu eneo hilo ambao umewaathiri pakubwa hali zao za kimaisha wengi wakiishi katika limbwi la umaskini.Hata hivyo wakaazi hao wanasema imekuwa vigumu kwa wao kupokea matibabu kutokana na bei ya dawa kuwa juu huku wengine wakikosa uwezo wa kununua dawa hizo.