HabariNews

Mshukiwa wa mauwaji ya wanawe wawili katika kaunti ya Mombasa amepatikana ameaga dunia kaunti ya Taita Taveta.

Mshukiwa wa mauwaji ya wanawe wawili katika kaunti ya Mombasa amepatikana ameaga dunia kaunti ya Taita Taveta.

Inakisiwa kuwa mshukiwa kwa jina la Jasson Chacha mwenye umri wa miaka 47 umepatikana ukining’inia kwenye nyumba moja katika kijiji cha Lesesia.

Chacha anadaiwa kuwauwa wanawe wawili Damel Jackson (8) na David Boke (4) katika wadi ya Ziwa la Ng’ombe, eneo bunge la Nyali kaunti ya Mombasa.

Katika ripoti ya upasuaji uliofanyiwa miili ya Watoto hao katika Hospitali ya Makadara imeonyesha kuwa Watoto hao waliuliwa kabla ya kuteketezwa.

Ripoti hiyo aidha ilibaini kuwa miili yao ilikuwa na majeraha ya moto ya kati ya asilimia 70 na 75.

BY EDITORIAL DESK