HabariNewsSiasa

PIGO KWA WA MBUNGE SIRISIA JOHN WALUKE.

Mbunge wa Sirisia John Waluke amepata pigo baada ya mahakama kufutilia mbali rufaa aliyowasilisha kupinga uamuzi wa mahakama ya ufisadi baada ya kupatika na hatia kufuatia madai ya ufisadi yaliyokuwa yakimkabili.

Jaji Esther Maina amemuagiza Walukhe na mhtakiwa mwenza na Grace Wakhungu kulipa faini ya shilingi bilioni 1 la sivyo ahukumiwe jela miaka 57.

Mbunge huyo ambaye alichaguliwa kwa mara nyingine kwa awamu ya tatu kati ka uchaguzi mkuu wa agosti 9 mwaka huu alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kupokea takriban shilingi milioni 297 za mahindi kutoka kwa bodi ya nafaka nchini NCPB mahindi ambayo yanadaiwa hayakusambazwa

Mwaka 2020 mahakama ya ufisadi ilimhukumu Walukhe miaka 57 gerezani baada ya kumpata na hatia ya kuiba shilingi milioni 297 pesa za bodi ya kitaifa ya nafaka na mazao NCPB.

Hata hivyo Walukhe alikata rufaa kupinga uamuzi huo.

Haya yanajiri huku

Mahakama kuu ikimkerejeshe mashtaka ya ufisadi wa shilingi milioni 60 aliyekuwa Waziri wa fedha Amos Kimunya.

Kimunya, na aliyekuwa mkurugenzi wa ardhi Lilian Njenga na mwenyekiti wa kampuni ya Midlanda ltd Junghae Wainaina waliondolewa mashtaka na hakimu Felix Kombo Juni mwaka wa 2021.

Upande wa mashtaka umeelezea kushangazwa na kuondolewa kwa mashtaka hayo.

Jaji Esther Maina amesema mahakama umeridhishwa na Ushahidi huo uliowasilishwa na upande na mashtaka ambao unaonyesha wazi watatu hao wana kesi ya kujibu hivyo kuwataka watatu hao kufika katika majengo ya mahakama tena kujitetea.

BY EDITORIAL TEAM