Inbox
Vita dhidhi ya ugojwa wa malaria ukanda wa pwani na maeneo ya nyanza vimepigwa jeki baada ya kuzinduliwa kwa mtego wa mbu unaotumia kawi ya miale ya jua unaolenga kukabiliana na maambukizi zaidi ya malaria nchini.
Mitego huo kwa jina MTego umezinduliwa na kampuni ya Engie Energy Access kwa ushirikiano na shirika la Uholanzi la PreMal na ni wenye muigo wa harufu ya mwanadamu ambayo huwavutia mbu na kunaswa.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la Engie Energy Access humu nchini Fredrick Noballa, amesema mtego huo ulioundwa kutumia teknolojia na hauchafui mazingira huku ukiwa na uwezo wa kuwanasa umbu wakiwa nje ya nyumba ili kuwazuia kuingia majumbani na kuathiri familia zilizolala au kubarizi.
Maeneo ya Pwani na Ziwa Victoria yameorodhesha kuwa maeneo yaliyo na mbu wengi, utumizi wa vyandarua ikiwa tengemeo la wengi huku kuzinduliwa kwa MTego kukilenga kutoa suluhu kamili mbadala wa utumizi wa vyadarua
Mwanzilishi mwenza wa kampuni ya PreMal Lorenzo Fiori amesema Kenya imetumia mabilioni ya fedha kukabiliana na maradhi ya Malaria katika miaka ya hivi karibuni, ila uwepo wa MTego huo wa umbu utakua suluhu katika kukabiliana na ugojwa wa malaria na kusaidia kuimarisha afya nchini
Kati ya shilingi bilioni 146.8 zilizotengewa sekta ya afya mwaka huu wa kifedha, shilingi bilioni 16 ziliengwa kukabiliana na maradhi ya Malaria, kifua kikuu na virusi vya ukimwi, hatua inayoonyesha athari ya ugojwa wa malaria na magojwa hayo mengine nchini
Takwimu kutoka shirika la Afya Ulimwenguni WHO zimeonyesha ongezeko la idadi ya vifo vitokanavyo na maradhi ya malaria nchini kutoka visa 11,768 mwaka 2020 hadi 12,011 mwaka 2021 huku ikivitaja visa vya maambukizi y a ugojwa wa maleria humu nchini kama asilimia 1.3% ya visa vyote vya malaria ulimwenguni.
BY EDITORIAL TEAM