Baadhi ya wakaazi walioibiwa vyombo vyao vya thamani kutoka mjini Kwale wamefanya maandamano ya amani wakishinikiza idara ya usalama kwale kufanya msako wa kuwatafuta wahalifu wanao hangaisha wenyeji wa eneo bunge la Matuga.
Wakiongozwa na Omar Mwadosho akithibitisha kuibiwa pesa taslimu laki tatu na nusu na vyombo vyengine vya umeme ndani ya nyumba yake.
Aidha Mwadosho ameendelea kusema kuwa visa vya wizi vimekithiri mno huku akiilaumu idara ya usalama kwa kutotilia maanani visa hivyo huku akitaja ushirikiano baina ya askari na wakaazi ukiwa changamoto kubwa kwao.
Kwa upande wao maafisa katika mashirika ya utetezi wa haki za kibinadamu,afisaa wa human rights ajenda (Huria) Alex Mwarua amesema kuwa kuna visa 50 kwa sasa vilivyoshuhudiwa kwenye jamii.
Wakaazi wameilaumu idara ya usalama kaunti hiyo Kwa kuzembea katika utendakazi wao huku ikipelekea visa vingi vya utovu wa usalama kukithiri katika baadhi ya maeneo.
BY EDITORIAL TEAM