HabariNews

NEMA tawi la kaunti ya Kwale imesema inashirikiana kwa karibu na kamati za ulinzi ili kudhibiti mifuko ya plastiki kuingia nchini.

Mamlaka ya mazingira nchini NEMA tawi la kaunti ya Kwale imesema inashirikiana kwa karibu na kamati za ulinzi pamoja na vitengo vya usalama katika maeneo ya mipakani ikiwemo eneo la Lungalunga kudhibiti mifuko ya plastiki kuingia nchini.

Mkurugenzi katika mamlaka hiyo Godfrey Wafula amesema japo kaunti ya Kwale imepiga hatua kubwa katika kufuata marufuku hiyo, kumekua kukishuhudiwa baadhi ya wakaazi wanaotumia mianya katika maeneo ya mipakani kuingiza mifuko ya plastiki kutoka nchi jirani ya Tanzania.

Wafula amesema tayari wameweka mikakati zaidi kudhibiti matumizi hayo ya mifuko ya plastiki hususan katika masoko ya mipakani huku akiwahimiza wakaazi wa kaunti ya Kwale kuzingatia marufuku hiyo iliyowekwa katika harakati za kuimarisha tena mazingira.

BY EDITORIAL DESK