HabariNews

Shirika la huduma la Kenya ferry services latakiwa kuainisha huduma zake katika kivuko cha Likoni ili kurahisisha usafiri kwa watalii.

Shirika la Kenya association of hotel keepers sasa wanalitaka shirika la huduma la Kenya ferry services kuainisha huduma zake katika kivuko cha Likoni ili kurahisisha usafiri kwa watalii wanaozuru eneo la Diani kaunti ya Kwale.

Mkurugenzi wa shirika hilo Sam Ikwaye anasema kwamba msongamano unaoshuhudiwa katika kivuko hicho huenda ukatatiza shughuli za kitalii kusini mwa pwani msimu huu wa sherehe za krismas.

Aidha amedokeza kuwa eneo la pwani limeandikisha asilimia 80 hadi 90 ya wageni huku kaunti ya kwale ikirekodi zaidi ya asilimia 90 msimu huu wa likizo ndefu.

Kwa upande wake Jeff Mkolwe meneja mkuu wa hoteli ya baobab resort and spa amethibitisha idadi kubwa ya wageni kutoka mataifa ya nje baada ya kuimarika kwa usalama kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

BY EDITORIAL DESK