HabariNews

Wafanyibiashara wanaoendeleza shughuli zao nje ya hospitali ya rufaa ya Msambweni watakiwa kuondoa hofu ya kuvunjiwa vibanda vyao.

Mwakilishi wa wadi ya Ramisi kaunti ya Kwale Hanifah Mwajirani amewataka wafanyibiashara wanaoendeleza shughuli zao nje ya hospitali ya rufaa ya Msambweni kuondoa hofu ya kuvunjiwa vibanda vyao na serikali ya kaunti hiyo.

Akizungumza huko Msambweni, Mwajirani amesema kuwa tayari bunge la kaunti hiyo limetenga fedha za ujenzi wa vibanda hivyo katika sehemu mbadala kupitia mpango wa ruwaza ya maendeleo ya mwaka 2023/2024.

Mwakilishi huyo amewahakikishia wafanyibiashara hao kwamba hawatavunjiwa vibanda vyao hadi pale serikali ya kaunti itakapowajengea vibanda hivyo kabla ya kuhamishwa kutoka eneo hilo.

Mwajirani ambaye pia ni kiongozi wa wengi katika bunge la Kwale amesema kuwa wafanyibiashara hao watapewa kipaumbele baada ya ujenzi wa vibanda vipya kukamilika ili kutoa nafasi kwa ujenzi wa barabara ya eneo hilo.

BY EDITORIAL DESK