HabariNews

Fatuma Masito amewataka wakaazi kutilia maanani umuhimu wa kupanda miti.

Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Kwale Fatuma Masito amewataka wakaazi kutilia maanani umuhimu wa kupanda miti.

Akizungumza katika kijiji cha Vigurungani , eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale Masito amesema kuwa ardhi kubwa ya eneo hilo ni jangwa kutokana na ukataji ovyo wa miti.

Akisisitiza kuwa tabia hiyo imepelekea kufukuza mvua huku eneo hilo likisalia jangwa kinyume na siku zilipopita ambapo ilikuwa msitu.

Masito amewataka wakaazi kushirikiana na viongozi ili kuregesha hadhi ya msitu ya eneo hilo.

Ameongeza kuwa matatizo ya baa la njaa yanayoshuhudiwa eneo hilo mara kwa mara ni kutokana ukosefu wa miti.

BY EDITORIAL DESK