HabariNews

Vita dhidi ya ukeketaji wa wasichana na wanawake nchini vimepigwa jeki nchini.

Vita dhidi ya ukeketaji wa wasichana na wanawake nchini vimepigwa jeki baada ya muungano wa wake wa magavana kushirikiana na shirika la umoja wa mataifa la UNFPA katika vita hivyo, muungano huo ukipania kuwalinda wasichana haswa msimu huu wa likizo ambapo wako nyumbani kwa kipindi kirefu.

Kaunti 22 humu nchini zinajihusisha na ukeketaji huku likizo hii ikiwa imewapa muda mwafaka baadhi ya wazazi katika kaunti hiyo kuendeleza tamaduni hiyo.

Kulingana na Alamitu Guyo Jattani ambaye ni mwenyekiti wa muungano wa wake wa magavana nchini anasema kuwa wazazi katika jamii zinazoshiriki ukeketaji hutumia fursa ya likizo kuendeleza tamaduni hiyo.

Ukeketaji ukifanyika katika jamii mbali mbali kwa sababu tofauti kulingana na itikadi na tamaduni ya familia hizo.’

kwa upande wake mshauri wa maswala ya kijinsia kutoka shirika la UNFPA Caroline Murgor amesema kuwa kuna umuhimu wa kuwahusisha wanaume kwenye swala hilo kwani wanajukumu kubwa kukabiliana na ukeketaji.

BY EDITORIAL DESK