HabariNews

Wito umetolewa kwa watakaokuwa wanatembelea fuo za bahari katika kaunti ya Kwale kufuata maagizo ya kuogelea.

Wito umetolewa kwa watakaokuwa wanatembelea fuo za bahari katika kaunti ya Kwale kufuata maagizo ya kuogelea ili waepuke visa vya watu kuzama msimu huu wa sikukuu ya krismas na mwaka mpya

Kulingana na Clara Mulwa ambaye ni mpiga mbizi katika kaunti ya Kwale wanatoa taarifa katika sehemu zote za ufuo zitakazokuwa na taarifa kuhusu watu kuwa salama wanapoogelea.

Pia amesema kuwa kutakuwa na wapiga mbizi watakaotoa msaada wa kuokoa maisha pindi itakapohitajika, Mulwa amewataka wazazi kuwa makini wanapokuwa kwenye fuo hizo kwani mara nyingi watoto hupotea kunapokuwa na idadi kubwa ya watu baharini.

Akiongeza kuwa ni muhimu wazazi wawe macho kuwaangalia watoto wao waapokuwa ndani ya maji ili kuepuka visa vya watoto kuzama.

BY EDITORIAL DESK