HabariNews

Ipo haja ya kuongezwa vituo vya polisi katika sehemu ya kombani na tiwi kama njia ya kuongeza usalama.

Ipo haja ya kuongezwa vituo vya polisi katika sehemu ya kombani na tiwi kama njia ya kuongeza usalama ikizingatiwa kwamba usalama sehemu hizo unaonekana kuwa changamoto.

Mbunge wa Matuga kaunti ya Kwale Kassim Tandaza ameahidi kutenga shilingi milioni 5.5 fedha za ujenzi wa kituo cha polisi katika maeneo ya Kombani na Tiwi kwenye mwaka wa bajeti ya kifedha wa 2022/2023.

Tandaza amesema kuwa analenga kutumia shilingi milioni 2 kutoka kwa hazina ya CDF kujenga kituo cha polisi cha Tiwi huku shilingi milioni 3.5 zikitumika kupandisha ngazi kituo cha Kombani.

Mbunge huyo amedokeza kwamba hatua hiyo inalenga kuboresha usalama katika maeneo hayo yaliyokithiri visa vya utovu wa nidhamu.

Kwa upande wake kamishna wa Kwale Gideon Oyagi amependekeza kuongezwa kwa idadi ya manaibu wa kamishna katika eneo bunge la Matuga.

Oyagi amesema kuwa maafisa hao watapelekwa kuhudumu katika sehemu za Tiwi na Waa/Ng’ombeni ili kuzidisha juhudi za kudumisha amani eneo hilo.

BY EDITORIAL DESK