AfyaHabariNews

Vituo 46 vya Afya vyafungwa Kaunti ya Mombasa

Vituo 46 vya afya Kaunti ya Mombasa vimefungwa kutokana na kukosa kuafikia viwango vinavyohitajika kutoa huduma za afya kwa umma.

Kulingana na Baraza la Wahudumu wa Afya KMPDC ukaguzi wa vituo 263 kati ya 436 vilivyosajiliwa ulifanyika ili kubaini iwapo vinafuata sheria.

Washukiwa 3 wamekamatwa wakati wa ukaguzi huo kwa kutokuwa na leseni za kuwakubali kufanya kazi na watasaidia katika uchunguzi.

Kaimu Mkurungezi Mkuu wa Baraza hilo Philip Ole Kamwaro amewashauri wananchi kutafuta huduma za matibabu katika vituo vya afya vilivyosajiliwa.

Kwa upande wake Mkurungezi msaidizi wa huduma za matibabu wa kaunti ya Mombasa Abdulmanaf Zein amesema ukaguzi huo utaendelea ili kuhakikisha watu wamepata huduma bora.

Zein ameongeza kuwa upungufu wa wafanyakazi katika vituo vya afya vya serikali umekua changamoto, japo amebaini kuwa ni suala ambalo watakabiliana nalo.