HabariNews

Washikadau wa kiusalama waelimishwa mbinu mbadala za kutatua migogoro

Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Yetu limeanza zoezi la kuwaelimisha washikadau mbalimbali wa usalama juu ya mbinu mbadala za kutatua migogoro ya kijamii.

Akizungumza katika ufunguzi wa zoezi hilo eneo bunge la Kisauni kaunti ya Mombasa, naibu kamishna eneo hilo Jamlick Mbuba ametaja kuwa elimu hiyo itachangia pakubwa katika masuala

mbalimbali ikiwemo kudumisha amani na umoja katika jamii sawia na kupunguza kesi mahakamani.

Kwa upande wake naibu chifu wa Majaoni Hakika Jacob amesema kuwa elimu hiyo itaboresha ujuzi wao zaidi wa kutatua kesi na migogoro mashinani.

Ikumbukwe kwamba idara ya mahakama imekuwa ikitilia mkazo wa kutumika kwa mbinu mbadala kutatua migogoro na kesi.

BY JOYCE KELLY