HabariNews

SHIRIKA LA MUHURI LATAKA JAMII KUELIMISHWA KUHUSU DHULMA ZA KIJINSIA

Mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu kutoka shirika la MUHURI Topista Juma amesema kuna haja ya jamii kuelimishwa kuhusu visa vya dhulma ya kijinsia ili kuepukana na visa hivi.

Topista amedokeza kuwa hali ngumu ya uchumi imechangia kuongezeka kwa visa hivi katika jamii.

Aidha Topista ameongeza kuwa  kuwa mara nyingi waathirika wa visa hivi hukosa kuripoti kutokana na umaskini unaowakumba.

“Ni masikitiko sana hasa wakati huu ambapo hali ya uchumi ni ngumu na dhulma za kijinsia zimeongezeka miongoni mwa wanajamii na haziripotiwi jinsi zinavyostahili ili tuweze kusaidiana, na watu wanaoripoti visa hivi mara nyingi ni watu wachochole wasiojiweza.”Amesema

Topista amesema shughuli ya kuripoti visa vya dhulma bado inakumbwa na changamoto ya kufuta sheria hasa upande wa kupata notisi kutoka kwa polisi.

Topista amehimiza wote wanaoshuhudia visa hivi kuripoti mapema hasa miongoni mwa watoto  akisema hatua hiyo itamwezesha mwathiriwa kujikwamua kwenye msongo wa mawazo hata athari nyingine nyingi za kiafya.

“Kwa wale wanaodhulumiwa na hawajitokezi mimi nitawaambia hiyo inazidi kuwaongezea  wa mawazo kumbuka unapozungumza na mwenzako unapunguza na unaponyamaza unazidisha yale mawazo.”Alikariri.

Topista amewaonya vikali wazazi waliona tabia ya kunyamazia san asana dhulma inapofanywa na mtu wa familia ama aliye na ukaribu naye akisema hatua hiyo inaongeza dhulma miongoni mwa watoto.

Wakati huo huo Topista amepongeza mahakama kuu kwa kuleta korti la kusuhisha kesi za kijinsia kaunti ya Mombasa akisema imesaidia pakubwa katika kukabiliana na visa hivyo

“Kwanza tunafurahi sana kwa Mahakam Kuu kwa kuleta korti ya jinsia katika kaunti ya Mombasa tunajivunia kuwa na korti ya kuskiza kesi za kijinsia na kesi hizi zinaporipotiwa zinaenda kwa haraka sana.”Amesema Topista.

BY EDITORIAL DESK