HabariNews

SERIKALI YAOMBWA KUWAHAKIKISHIA USALAMA WALIMU WALIOKO KWENYE MAENEO YANAYOSHAMBULIWA MARA KWA MARA

Katibu wa Muungano wa walimu Tawi la Kilindini Dan Aloo amehimiza serikali kuu kufanya jitihada  ili kuhakikisha usalama wa walimu hasa kwenye maeneo ambayo yanashuhudiwa mashambulizi ya mara kwa mara unaimarishwa.

Akizungumza na meza yetu ya habari Aloo amesema mashambulizi yanapotokea huzuia walimu kukubali kuenda katika shule za maeneo hayo wakati wa uhamisho wakihofia usalama wao.

Aidha Aloo ametaja hali hiyo kuchangia kudhorora kwa masomo ya wanafunzi kutokana na uhaba wa walimu wenye tajriba ya hali ya juu.

“Nataka serikali ifanye uchunguzi wakati walimu wanataka kuajiriwa kuna wale ambao wanajifanya ni Al-shaabab lakini ni magaidi wa kijamii wanataka  kuwatawanyisha watua ambao wako tayari kuwasaidia.”Amesema Aloo

Aloo ameongeza kuwa walimu wanafaa kuwa wamechanganyika  shuleni kuhakikisha kila somo lina mwalimu wake na hali ya kutokuwa na utulivu huchangia uoga kwa walimu wengi.

Wakati huo huo Aloo ametaka wenyeji wa maeno hayo kuwa makini na kuripoti visa vya ugaidi akisema ni sharti jamii ishirikiane na vitengo vya usalama katika maswala ya kuimarisha viwango vya elimu maeneo hayo.
“Jamii ambazo ziko maeneo hayo waangalie jinsi ya kuwasaidia watu wao mahali kama Msitu wa Boni kunapotokea mlipuko masomo hayawezi kuendelea kuna yale mazingira ambayo hayaendi na masomo.Alisistiza.

Aloo ameongeza kuwa hali hiyo inadhororesha viwango vya masomo maeneo hayo.

“Kama mko na shida  serikali fanyeni mazungumzo tumeweka jitihada ili kuhakikisha watoto wanafaulu.”Amesema.

BY EDITORIAL DESK