HabariNews

Mwili wa aliyejirusha darajani Kilifi wapatikana

Mwili wa mwanamume anayedaiwa kujirusha kwenye daraja la Kilifi umepatikana katika ufuo wa bahari hindi mjini humo mapema siku ya jumatatu.

Polisi mjini Kilifi walisema walipata taarifa kutoka kitengo cha usalama wa baharini kuhusu tukio hilo lililofanyika jumapili jioni.Kulingana na polisi baadhi ya vungo vya mwenda zake vilikuwa vimevunjika, kutokana na hali ya  kujirusha kutoka juu ya daraja hilo.

Naibu wa kamanda wa polisi eneo bunge la Kilifi kaskazini Esther Mwendwa, alithibitisha tukio hilo na kuongeza kuwa kufikia sasa bado mwili huo haujatambuliwa.

Mwendwa aliwasihi wakazi kutafuta ushauri nasaha wakiwa wanapitia changamoto za kimaisha ambazo mara nyingi husababisha matatizo ya akili.

Polisi huko Kilifi walisema wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha tukio hilo.

BY ERICKSON KADZEHA