HabariNews

Haki Afrika yashinikiza serikali kulipa waathiriwa  Fidia

Mashirika ya kutetea haki za binadam hapa pwani yanaiomba serikali kuu kuwalipa fidia wahanga wa shambulizi la kigaidi lililofanyika mwaka wa 1998 katika ubalozi wa marekani jijini Nairobi.

Afisa wa shirika la Haki afrika Mathias Shipeta alisema waathiriwa wa shambulio hilo wamekuwa wakiishinikiza serikali kulipwa fidia bila mafanikio licha ya kupitia mahangaiko.

Afisa huyo vile vile aliongeza kuwa fidia hiyo huenda ikwasaidia katika shuguli zao za maisha.

Wakati huo huo Shipeta ameshinikiza serikali kuweka ulinzi Zaidi sehemu za mipaka ili kuhakikisha inakabiliana na magaidi wanaotekeleza mashambulizi hapa nchini.

Haya yanajiri wakati Kenya na Tanzania zikiadhimisha miaka 25 tangu mashambulizi mabaya zaidi ya kigaidi kufanyika katika mabalozi ya marekani jijini Nairobi na Dar es alam mwatawalia.

Hapa nchini watu 224 waliaga dunia huku zaidi ya wengine 4,000 wakijeruhiwa baada shamulizi hilo la ubalozi wa Marekani jijini Nairobi.

Mashambulizi hayo yalihusishwa moja kwa moja na kundi la kigaidi la Alkaida wakati huo likiongozwa na Osama bin laden ambaye aliuwawa mwaka 2011.

Mashambulizi hayo yalitokea tarehe 7 agosti mwaka 1998.

BY EDITORIAL DESK