HabariLifestyleNews

Wizara ya Elimu Kuchukulia Hatua Kali Shule Zinazozuia Wanafunzi kuvaa Hijabu

Wizara ya elimu nchini imeahidi kuanzisha uchunguzi ili kuzitambua shule zinazowazuia wanafunzi wa kike kuvalia vazi la hijab.

Waziri wa elimu Ezekiel Machogu amekemea hatua hiyo akiitaja kuwa kinyume cha katiba huku akisema kuwa kila mwanafunzi ana uhuru wa kufuata mismamo yake ya kidini bila kubaguliwa.

Machogu ameeleza kuwa wizara yake imewasilisha agizo kwa Wakurugenzi wa Idara ya elimu katika kaunti zote nchini ikiwataka wahakikishe kwamba wanatambua na kufuatilia kwa ukaribu visa vyovyote vya ukiukaji wa uhuru wa kidini katika meneo yao.

Haya yanajiri baada ya kauli ya seneta mteule kaunti ya Mandera Mariam Sheikh kudai kuwa baadhi ya wanafunzi wa kiislamu wamekuwa wakizuiliwa kuvalia hijabu shuleni na kuwapelekea kuhamia katika shule zinazoendana na misimamo yao ya kidini.