HabariNews

Rais Ruto aisihi Jumuiya ya Afrika Kusitisha Mipango ya Mapinduzi ya Kijeshi

Baadhi ya viongozi wa Afrika wamesihi wananchi wake kusitisha mipango ya mapinduzi ya kijeshi ambayo yamekuwa yakishuhudiwa katika mataifa ya Afrika Magharibi na kukumbatia demokrasia.

Akihutubia wanadiplomasia na wawekezaji katika jiji la Maputo nchini Msumbiji rais william Ruto ameeleza kuwa mapinduzi ya kijeshi huchangia maafa na uharibifu wa uchumi hivyo basi kuna haja ya swala hilo kuangaziwa zaidi na miungano ya Afrika na Ulaya.

Ruto amesema wanachama wa Umoja bara Afrika AU hawaungi mkono mapinduzi ya kijeshi kwenye mataifa yanaoangazia demokrasia na kusisitiza kwamba mapinduzi hayo sio suluhu ya changamoto wanazopitia waafrika.

“Kama Muungano wa Umoja wa bara la Afrika tunapinga kuondolewa kokote kwa serikali iliyochaguliwa kidemokrasia, Mapinduzi si suluhu kwa changamoto tulizo nazo kama bara la Afrika na ni kinyume cha demokrasia kama sera za kikoloni. Tunachukua msimamo mkali kama AU kuondolewa ungozini kwa kiongozi kinyume cha demokrasia kutapelekea nchi hiyo kuvuliwa uanachama wa AU.

Wakati huo huo Ruto amesema serikali yake imejitolea kushirikiana kibiashara kwa kwa karibu na taifa la Mozambique ili kuimarisha uwiano mzuri kati ya mataifa haya mawili.

BY EDITORIAL DESK