HabariNews

Umbali Wa Shule Kinango Miongoni mwa changamoto za Elimu.

Umaskini na uhaba wa shule za upili  eneo bunge le Kinango kaunti ya Kwale umetajwa kuwa changamoto kuu ya idadi ndogo ya wanafuzi wanaojiunga na kidato cha kwanza baada ya kukamlilisha masomo ya msingi.

Katibu wa chama cha KNUT tawi la Kinango Moses Mzungu alisema umbali wa shule za upili eneo hilo umeathiri pakubwa elimu eneo hilo jambo ambalo alilitaja kufanya eneo hilo kusalia nyuma kimaendeleo.

Mzungu alipongeza serikali ya kaunti ya Kwale kwa ushirikiano na mashirika mbali mbali kwa juhudi ambazo wanafanya ili kuimarisha viwango vya elimu maeno ya mashinani akisema hatua hiyo itapunguza umaskini miongoni mwa jamii.

”Kuna changamoto ya shule eneo hilo ziko mbali kwa mfano unaweza ukakuta kata ndogo moja unaweza ukapata shule ya sekondari ni moja tu na iko karibu kilomita 25 mbali na mahali mwanafunzi anaishi .”amesema Mzungu.

Mzungu alitolea mfano eneo la Busho ambako kulikuwa na changamoto ya ukosefu wa shule ya upili akidokeza kuwa kupitia viongozi wa kisiasa kwa ushirikiano na mashirika mbali mbali  waliweza kujenga shule ya upili ambayo itasaidia pakubwa wanafunzi kutoka eneo hilo.

Wakati huo huo Mzungu alipongeza wazazi eneo hilo kwa kukumbatia elimu bila ubaguzi wa jinsia akodokez kuwa idadi ya wanafunzi wa kike eneo hilo imepiku ile ya kiume.

“Nashukuru wazazi eneo hilo kwa sababu sahii kila mzazi wanachukulia watoto wote kuwa sawa na wanafunzi wote wanapelekwa shuleni nahata sana sana ukiangalia idadi ya wanafunzi shuleni wengi wao ni wakike.”Amesema Mzungu.

Aidha Mzungu aliongeza kuwa ni wakaati sasa kila mzazi anafaa kuwa na ufahamau kuhusu elimu kwa kila mtoto bila ya kubagua jinsia yake na kumchukulia kila mwanafunzi kuwa sawa na mwengine.

BY NEWS DESK.