FoodHabariNews

GMO NI SALAMA! Mahakama Yapuuzilia mbali Kesi Ya Kupinga Kilimo na Uagizaji wa Vyakula vya GMO

Mahakama ya mazingira ikiongozwa ni jaji Oscar Angote imetupilia mbali kesi iliyowasilishwa kupinga kilimo na uagizaji wa vyakula vya kisaki (GMO) kutoka nje.

Kulingana na Angote, hakuna ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa kilimo cha ukuzaji wa vyakula hivyo unaweza kudhuru afya ya binadamu au mazingira, akisisitiza kwamba taasisi husika za humu nchini na za  kimataifa zina uwezo wa kutosha kudhibiti hali hiyo.

Angote aidha alithibitisha ubora na salama ya vyakula hivyo huku akipinga dhana kuwa henda lishe hizo zina kemikali hatari kwa afya ya binadamu na mazingira.

Haya yamejiri baada ya serikali kuamuru uagizaji na ukuzaji wa vyakula hivyo nchini ili kukabiliana na janga la uhaba wa chakula nchini.

BY EDITORIAL DESK