HabariNews

Muturi Azitaka Kampuni Kuwasilisha Majina ya wamiliki wao Halali

Kampuni  zinazohudumu humu nchini bila kusajili majina ya wamiliki halisi zinahudumu kinyume na sheria, hii ni kauli ya Mwanasheria mkuu Justin Muturi akiiambia kamati ya bunge la kitaifa kuhusu kawi.

Katika mazungumzo yake mbele ya kamati hiyo Muturi alisema kuwa sheria kuhusu usimamizi na usajili wa kampuni ipo wazi na sharti wote wanaokiuka sheria hiyo wachukuliwe hatua za kisheria.

Si wazi kwa msajili wa kampuni kujitokeza mbele ya bunge kusema usajili ulifanyika kitambo . ikiwa kuna kampuni yoyote ambayo haija wasilisha majina ya wamiliki wao inakiuka sheria iliyowekwa” alisema

Muturi hata hivyo aliitaka kamati hiyo kusajili wa kampuni na iwapo kuna ambazo zinakiuka sheria ziwajibishwe kwa mujibu wa sheria.

BY MEDZA MDOE