HabariLifestyleNews

Sherehe Sokoni Gatundu, rais mstaafu Uhuru Akiadhimisha Miaka 62

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa Oktoba 26, akigonga miaka 62 tangu kuzaliwa kwake.

Hii itakuwa mara ya pili kwa kiongozi huyo  kusherekea siku yake ya kuzaliwa nje ya uongozi ikiwa ni mwaka mmoja umepita baada ya kuipungia mkono wa kwaheri ikulu.

Shangwe na nderemo zilisheheni katika mji wake wa nyumbani kule  Gatundu ambako  wachuuzi katika soko kuu la eneo hilo walituma bishara njema kwa mstaafu rais huku wakimmiminia  sifa kede kede kiongozi huyo wa zamani huku wakiusifia uongozi wake kupitia nyimbo. Wakaazi hao walimsifia kinara huyo wakisema mambo yalikuwa shwari chini ya utawala wake kinyume na hali ilivyo kwa sasa.

Licha ya kiongozi huyo kutokuwepo sherehe hazikusistishwa kwani wachuuzi hao waliyabeba mabango yake yenye ujumbe wa kumuombea afya njema huku vyakula na vinywaji vikigawanywa kwa wote katika soko hilo.