HabariNews

Ziara ya mfalme Charles wa Uingereza Kenya yaandamwa na Jinamizi la historia ya Ukoloni

Rais William Ruto ameongoza hafla ya kuwapokea rasmi Mfalme Charles III na mkewe Malkia Camilla katika Ikulu ya Nairobi.

Licha ya kuwasili kwao nchini saa nne unusu usiku wa Oktoba 30, 2023 hakukuwepo na picha za kuonyesha wawili hao pamoja na ujumbe wao waliposhuka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JKIA.

Wawiili hao Walikaribishwa kwa kukagua gwaride la heshma kisha baadaye Rais Ruto akawaongoza kutekeleza zoezi la upandaji wa miche katika ikulu hiyo.

Mfalme Charles huwenda akakabiliwa na miito iliyoenea ya kuomba radhi ikiwemo hisia mseto kutoka kwa baadhiya jamii na makundi ya kutetea haki kutokana na historia ya awali ya ukoloni wa taifa la Uingereza.

Ziara ya Mfalme Charles III na Malkia Camila hata hivyo inatarajiwa kutoa fursa siku za usoni na kujenga uhusiano thabiti kati ya jiji la London na Nairobi.Ubalozi wa Uingereza ulitilia mkazo suala hilo Ulishikilia kuwa ziara hio itaangazia zaidi ushirikiano thabiti unaoendelea kati ya UK na Kenya.

Familia hii ya kifalme itakuwa nchini hadi tarehe tatu na wanatarajiwa kuzuru maeneo tofauti ikiwemo mji wa Mombasa, pamoja na kufanya mazungumzo na Rais William Ruto, Viongozi, makundi tofauti pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali.

BY EDITORIAL DESK