HabariNews

Miaka 60 baada ya Uhuru wakazi wa Wasini na Mkwiro Wapata Nguvu za Umeme

Wakazi wa kisiwa cha Wasini kaunti ya Kwale wana kila sababu ya kutabasamu kutokana na mradi wa usambazaji wa nguvu za umeme kuwafikia.

Kulingana na mwenyekiti wa Shirika la usambazaji umeme vijijini Rerec, Godfrey Lemio, nijukumu lao kuhakikisha sehemu mbalimbali za taifa zinanufaika na nguvu za umeme.

Inaarifiwa kuwa familia zaidi ya elfu 4,000 zinatarajiwa kunufaika na mradi huo baada ya kisiwa hicho kilichosalia kwa miongo 6 bila nguvu za umeme. familia 615 zikitarajiwa kunufaika na usambazaji huo katika awamu ya kwanza.

“ Ni jukumu letu kama REREC kutoa nguvu za umeme kwa sehemu zote za umma na tunafahamu kuwa Kwale ni sehemu ya kenya, kwahi ni jukumu letu kuhakikisha kuwa nchi nzima hasaa sehemu za mashambani zinapokea umeme tukiangazia kwamba sehemu hii imetelekezwa tangu taifa lipate uhuru. Hapa tunalenga takriban 4,000 sababu takwimu za watu katika kisiwa ni takriban 4000.” Alisema

Kwa upande wake Alivian Shamanga mkaazi wa eneo hilo aliupongeza mradi huo akisema utawafaa kwa mambo mbalimbali. Eneo la Mkwiro pamoja na Wasini hata hivyo zikitarajia ikupokea kutumia mradi huo kuanzia mwezi ujao.

Nashkuru sana mpaka muda huu naona dalili kwamba moto utakamilika ili tupate kuwasha na mimi nifurahie. Nimenunua TV miaka 35 iliyopita lakini tunatumia battery na sola hizi ndogo ndogo, kwahio ukija moto pia ntafurahia maana wajukuu wangu na wanagu watakua wanafurahia.” Alisema

BY EDITORIAL DESK