HabariMombasaNews

Raila Amtaka rais Ruto Kuunga mkono Umoja wa Mataifa Kutetea Haki za Wapelestine

Kinara wa Azimio Raila Odinga amemkashifu Rais William Ruto kwa kukaa kimya kuhusiana na vita vinavyoendelea baina ya taifa la Israel na Palestine.

Akiongea huko Port Rietz hapa mjini Mombasa wakati wa uzinduzi wa Shehena ya dawa, Odinga alisema Wapalestina wana haki kama binadamu wengine. Raila alimtaka rais Ruto kuvunja kimya chake kufuatia vita vinavyoendelea na kuungana na umoja wa mataifa kutetea haki za wapestine.

“Israel wacha kupiga watoto na akina mama ambao hawana hatia, Serikali ya Kenya mpaka ichukue msimamo, bwana Ruto amekaa kimya, wale Wapalestina vile vile ni binadamu ndio tunaambia bwana Ruto wewe huna msimamo kama vile ya bara Afrika AU imetoa taraifa Palestina ambao wanauawa kiholela na serikali dhalimu ya Israel,” Alisema Odinga.

Wakati uo huo Odinga aliishinikiza serikali ya Kenya Kwanza kutimizia ahadi zake walizozitoa kwa wananchi wakati wa kampeni badala ya kuendelea kutoa ahadi nyingine.

Akiongea mjini Mombasa Odinga alisema suala la gharama ya maisha lingali tete na linalomwumiza mwananchi hivyo kushinikiza serikali kukoma kulifumbia macho.

“Serikali kuu itekeleze wajibu wake badala ya maneno tupu domo kaya, bei ya unga , sukari, stima iko juu, wananchi wanalala njaa bila chakula, badala ya kuzuru hapa na pale maneno matamu na ya porojo wananchi wanaumia ndio sababu nawaambia wana jukumu sio kuleta porojo,” Alisema.

Kinara huyo wa AZIMIO aidha alisisitiza haja ya kuweka maslahi ya wakenya mbele akidokeza kuwa muungano wa Azimio hauwezi kuweka mkataba kama maswala ya wakenya hayajapewa kipaumbele. Alisema kuwa Muungano huo hautafanya mkataba wa makubaliano na Kenya Kwanza iwapo suala la gharama ya maisha na maswala muhimu ya Wakenya hayataangaziwa.

“Sisi kama Azimio hatuwezi kwenda kufanya mkataba yoyote ambayo haitaweka mambo ya huduma ya wananchi juu na kupunguza gharama ya maisha halafu yale mengine vile vile yafanyike kukagua kama vile sava na kadhalika tunasema hiyo hatuwezi,” Alisema

Odinga hata hivyo aliwataka viongozi wa Kenya Kwanza kukoma kutoa ahadi hewa badala yake kufanyia wakenya kazi akiwataja bado wakenya wengi wanahangaika kwa kupanda kwa bei ya bidhaa.

MJOMBA RASHID