HabariNewsSiasa

Gavana Mwangaza Akwepa Shoka la Mchujo, Wawakilishi wadi wakisalia Kusutwa

Wakilishi wa bunge la Meru wamesutwa kutokana na madai waliyoibua dhidi ya Gavana wa Meru Kawira Mwangaza saa chache baada ya gavana huyo kunusurika  jaribio la kumbaduliwa mamlakani.

Gavana huyo alikwepa shoka la kubanduliwa kwake kutokana na madai ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya rasilimali za Kaunti ya Meru, uteuzi kinyume na sheria na kutoa majukumu kwa afisi, madai ya kudharau bunge la kaunti na pia mahakama miongoni mwa madai mengine.

Akizungumzana na sauti ya Pwani kwa njia ya simu wakili tajika Luke Mukathe aliwasuta wakilishi wadi hao kwa kuibua madai ambayo walifeli kuyathibitisha mbele ya bunge la seneti.

Kulingana na Wakili Luke hoja za mawakili wa bunge la kaunti ya Meru waliongozwa na Muthomi Thiankolu zilisheheni siasa za ubabe za kaunti hiyo badala ya ithibati ya kutosha kuunga mkono madai yaliyoibuliwa dhidi ya gavana mwangaza.

Kwanza madai waliokua nayo baadhi yalikinzana na mengine yalikuwa madai ya kisiasa yaliyokosa msingi wa sheria na hawakufikia jukwaa mwafaka kwa njia zinazostahili. Tatizo kuu lao ni kwamba baadhi ya madai yao yalikuwa kweli na baadhi hayakuwa yakweli na pia madai hayo ya kweli hayakuelezwa inavyostahili. ” Alisema

Wakati huo uo, wakili Mukathe alisema kuwa madai yaliyoibuliwa dhidi ya aliyekuwa mbunge mteule wa EALA na Tigania Mashariki Mpuru Aburi yalibadiri mkondo mzima wa kumuondoa gavana huyo ofisini.

Ilibadili kwa njia kubwa sana kwa sababu alileta picha ya kwamba wanawake hawana nafasi, alithibitisha kwamba lolote waliokuwa wakifanya si kwaniaba ama uzuri wa Meru kama kaunti.iyo ilichangia pakubwa manake ukisikiliza wabunge walipokuwa wakitoa maoni yao walisema wanawakilisha dada zao, mama zao, wake zao dada zao na mabibi zao”alisema

Wakili huyo hata hivyo aliendelea kwa kutoa wito kwa Gavana Mwangaza na wakilishi wadi wa Meru kushirikiana ili wafanyie kazi pamoja wakaazi wa kaunti hiyo.

Kawira Mwangaza atulie,awaite maMCAs wake waketi wazungumze watafute njia mwafaka ya kutatua matatizo yao na waendelee na uongozi” alisihi wakili Luke

Itakumbukwa kuwa madai yote ya yaliyoibuliwa na wakilishi wadi wa kaunti ya meru yaligonga mwamba kwa kukosa ushahidi wa kutosha wa kuyaunga mkono madai waliyoibua dhidi ya gavana mwangaza.

Isaiah Muthengi