Zaidi ya wajumbe 1000 wanatarajiwa kuhudhuria kongamano la tano la jumuiya ya kilimo biashara na uchumu samawati ili kujadili maendeleo ya kuwa wenyeji wa JABEIC mwaka 2023.
Kulingana Emmanuel Nzai mkurugenzi mtendaji wa jumuiya ya kaunti za pwani, kuwepo kwa shirika moja la kaunti za pwani ambalo litaweza kuleta wawekezaji (Mombasa Investment Cooperation) ambalo litatumika kama kidhibitisho kwa wawekezaji kwamba eneo la pwani liko tayari kwa uwekezaji.
“Shirika la kuleta uwekezaji mombasa investiment cooperation na ambayo jumuiya tumekuwa tukishughulikia katika hii miaka karibu mitano na iyo ndio mojawapo ambayo tutaonyesha wawekezaji kwamba tuko tayari kabisa kufanya biashara na tunavifaa maalum ambayo vimetengenezwa ili kufanya hii biashara na uwekezaji rahisi.” Alisema Nzai
Kwa upande wake Mohammed Osman waziri wa utalii, biashara na utamaduni kaunti ya Mombasa alilitaja kongamano la Jumuiya Agribusiness and Blue Economy Investiment (JABEIC) ambalo litafanyika kati ya tarehe 28-30 mwezi huu wa Novemba litaweza kuimarisha uchumi na biashara kwenye kaunti hii.
“Tunahakikisha kuwa hwa wanabishara pia wanapata nafasi ya kujua biashara gani ambayo inaendelea hapa mombasa, na vitu tutakavyozungumzia ni nafasi za kujumuika kwenye kongamano hili na kuonyesha upeo wao.” Alisema Osman
Kauli zao zilipigwa jeki na mkurugenzi mkuu mtendaji wa shirika la Mombasa Investment Cooperation Swahali Bawaziri amesema kongamano hilo litawezesha kaunti zote sita za ukanda wa pwani kushirikiana na kuwekeza kwa pamoja.
“Sisi ndio shirika la uwekezaji Mombasa, na umuhimu wa hili kongamano ni kuhakikisha tunafanya kazi kwa pamoja kama miji ya ukanda wa Pwani na kauli mbiu ya mwaka huu ni ukulima na uchumi samawati” Alisema Bawaziri