HabariNews

Martin Dzombo Aidhinishwa Kuwa Nahodha wa meli ya KMA

Katibu mkuu katika wizara ya madini na uchumi sawamati Godfrey Kaituko alimuidhinisha rasmi Martin Munga Dzombo kuwa mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya maswala ya ubahari-KMA kaunti ya Mombasa.

Kulingana Godfrey, hatua hii ilijiri baada ya makubaliano ya bodi ya mamlaka hiyo kwa ushirikiano na wizara hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kaituko alimtaja Dzombo kuwa mwenye uzoefu na maswala ya kazi akisema ataleta manufa makubwa katika mamlaka hiyo.

Bw Martin Dzombo amechanguliwa kuw mkurugenzi mkuu wa mamlaka hii kama manvyojua ana uzoefu wa kazi na mataifa ya nje na tunaamini ya kuwa ataleta manufaa makubwa kwa mamlaka hii kwa kuleta wataalamu mbali mbali kwenye sekta hii.” Alisema Kaituko.

Kwa upande wake Dzombo alisema jukumu lake ni kuaanzisha nguvu mpya katika mamlaka hiyo kupitia uwekezaji wa kibinafsi pamoja na kuendeleza ajenga za vijana kwenye kazi za ubaharia hali itakatoa nafasi za ajira humu chini.

Jukumu langu hapa ni kuanzisha nguvu mpya katika mamlaka hii ili kuhimiza uwekezaji na uwekezaji wa kibinafsi na kutoa mwaongozo wa mifumo ya kisasa ya uwekezaji ili kukuza sekta hii pamoja na kushirikiana na washikadau mbali mbali ili kutoa nafasi za kazi humu nchini.” Alisema Dzombo.

Naye mwenyekiti wa mamlaka ya KMA kaunti ya Mombasa Hamisi Mwaguya alisema taifa lina uwezo mkubwa katika maswala ya bandari akiahidi kuwa kama bodi watashirikiana na kufanya kazi pamoja.

Taifa lina uwezo mkubwa katika sekta ya maswala ya ubaharia na tunaamini ya kuwa kiongozi wetu ataweza kushirkiana na washikadau katika sekta hii kuimarisha sekta hii na nataka kukuhakikishia kuwa tuko na wewe kuhakikisha tunafanya kazi pamoja.” Alisema Mwaguya.

By Medza Mdoe