Wito umetolewa kwa idara ya usalama nchini kuimarisha hali ya usalama katika ukanda wa Pwani hasa kaunti mombasa ambayo visa vya utekaji nyara vimekithiri kila kukicha.
Akizungumza na meza yetu ya habari katika mahojiano ya kipekee katibu mkuu wa baraza la maimamu na waubiri nchiini CIPK Sheik khalifa Mohammed amesema kuwa kwa sasa sio wakati wa kulaumia wala kujadiliana kwani ikizangatiwa kuwa maisha ya wengi yanapotea katika njia tatanishi mikoni mwa watekaji nyara.
Kwa upande wake sheik Mahmood Abdulahi amewasihi wazazi kuwa makini na watoto wao hasa nyakati hzi ambazo visa hivyo vinaendelea kushuhudiwa nchini huku akitoa tahadhari kwa kila mmoja kujichunga wakati huu umma umejawa na hasira kutokana na uhalifu huo.