Naibu kamishna wa eneo bunge la Msambweni kaunti ya Kwale Kipkech Lotiatia amewataka wazazi kaunti hiyo kuwalinda watoto wao kutokana na utumizi wa dawa za kulevya wakati huu wa likizo ya Disemba.
Akizungumza huko Msambweni, Lotiatia amewaonya wazazi dhidi ya kuwaachilia wanao hasa msimu huu wa sherehe za krismasi ili kuwaepusha na utumizi wa mihadarati.
Naibu huyo wa kamishna amedokeza kwamba eneo hilo linaongoza kwa utumizi wa dawa hizo kutokana na hatua ya wageni kuzuru eneo hilo la kitalii.
Kwa upande wake mbunge wa Msambweni Feisal Bader amesema kuwa idadi ya vijana walioathirika na mihadarati imeongezeka kwa kiwango kikubwa.
Hata hivyo, Bader amewaonya vijana katika eneo hilo dhidi ya kutumia dawa za kulevya kwa kisingizio cha ukosefu wa ajira.
BY NEWS DESK