Serikali ya kitaifa imesema kuwa itaendelea na shughuli ya kugawanya chakula cha msaada katika maeneo yaliyoathirika kaunti ya Kwale.
Kulingana na naibu kamishna wa eneo la Lungalunga Joseph Sawe ni kuwa eneo hilo ni miongoni mwa maeneo ambayo yanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na kiangazi cha muda mrefu.
Sawe akisema kuwa kutonyesha kwa mvua katika sehemu hiyo kumefanya wakulima wengi wa eneo hilo kukosa mazao.
Sawe ameongeza kuwa pia serikali inapeana kipaumbele katika sehemu za Lungalunga ambazo zimeathirika zaidi na baa la njaa.
Akisema kuwa serikali kuu, serikali ya kaunti pamoja na washikadau wengine wanashirikiana kuhakikisa kuwa wananchi wanaohitaji msaada huo wanapata chakula hicho.
BY NEWS DESK