HabariNews

Sherehe zenye ngoma za usiku zimetajwa kuwa chanzo cha mimba za mapema na dhulma zengine za kijinsia.

Sherehe zenye ngoma za usiku zimetajwa kuwa chanzo cha mimba za mapema na dhulma zengine za kijinsia.

Akizungumza eneo bunge la Shimba Hills kaunti ya Kwale naibu wa kamishna Moses Karwigi amepiga marufuku sherehe zote zilizo na nia ya kueka ngoma za usiku kuwa yeyote atakaye enda kinyume na agizo hilo mkono wa sheria utachukua nafasi yake inavyostahili.

Kamishna huyo amewaonya vikali wakaazi wa eneo bunge hilo dhidi ya disko matanga sawia na harusi zinazochezwa nyakati za usiku kuwa vijana wengi hutumia fursa hiyo kuendeleza uovu katika jamii.

Amesisitiza haja ya wazazi kuwachunga watoto wao wanapofunga kwa likizo la msimu wa Disemba akisema kuwa watoto wengi hutumia muda huu kuharibika.

BY NEWS DESK