HabariNews

Zaidi ya familia 1400 kutoka eneo la Maji ya Chumvi huko Kinango kaunti ya Kwale zinaishi kwa hofu kufuatia utata wa ardhi

Zaidi ya familia 1400 kutoka eneo la Maji ya Chumvi huko Kinango kaunti ya Kwale zinaishi kwa hofu kufuatia utata wa ardhi uliopo baina yao na mwekezaji wa kibinafsi.

Wakaazi wa eneo hilo wamemtaka rais William Ruto kuingilia kati kwani wana wasi wasi kuwa huenda ardhi zao zimenyakuliwa na mabwenyenye.

Wakiongozwa na Fredrick Kanato, wakaazi hao wanahofia kudhulumiwa endapo ardhi hiyo yenye utata ya ekari elfu 60 itagawanywa.

Wakaazi hao wamedai kwamba baadhi ya viongozi wao wanashirikiana na maafisa wa idara ya ardhi ili kuigawanya ardhi hiyo kinyume cha sheria.

Sasa wanamtaka rais anayezuru kaunti hiyo leo kuingilia kati na kusitisha shughuli zozote kwenye ardhi hiyo waliyoirithi kutoka kwa mababu zao.

BY EDITORIAL DESK