HabariNews

Serikali ya kitaifa inanuia kuweka mipango kikamilifu kuhakikisha kuwa wewekezaji mbalimbali wanaweza kufaidika kupitia biashara zao

Serikali ya kitaifa inanuia kuweka mipango kikamilifu kuhakikisha kuwa wewekezaji mbalimbali wanaweza kufaidika kupitia biashara zao sawia na kutengeneza nafasi za ajira mingoni mwa wakaazi katika maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza katika kijiji cha Gora eneo la Samburu kaunti ndogo ya Kinango wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza vyuma cha DEVKI STILL kilichogharimu bilioni 30 Raisi wa Kenya dr William Ruto amefichua kwa tayari amefanya mazungumzo na Raisi wa Uganda Yoweri Museveni li kusaidia kampuni hio kupata malighafi.

Hata hivyo viongozi wa kaunti ya Kwale waitaka kampuni hio kuangalia maslahi ya wakaazi katika nafasi za utoaji wa ajira .

Kwa upande wake mwenyekiti wa kampuni hio Nahendra Naval amesema kuwa tayari kampuni hio imeajiri watu elfu moja huku asilimia kubwa ikiwa ni ya wakaazi wa eneo hilo.

Kampuni hio inararajiwa kuanza shughli zake rasmi mwezi January mwaka ujao ambapo wakaazi 2500 wanatarajiwa kunafaika na nafasi za ajira.

BY EDITORIAL DESK