HabariNews

Rais William Ruto amewaonya vikali wanaojihusisha na biashara ya utumizi wa mihadarati.

Rais William Ruto amewaonya vikali wanaojihusisha na biashara ya utumizi wa mihadarati akisema kuwa serikali imejipanga kikamilifu kuwakabili.

Akizungumza eneo la Samburu kaunti ya Kwale Ruto ameelezea masikitiko yake jinsi vijana wengi wamekosa mwelekeo kutokana na utumizi wa mihadarati.

Ruto hata hivyo amefichua kwamba serikali imebuni njia ya kuwakamata wanaosafirisha madawa ili kuhakikisha kuwa wanaregesha hadhi ya wakenya.

Akigusia swala la pombe Raisi amesema kuwa kuwa serikali yake itapiga marufuku pombe haramu ambayo imeonekana kuleta madhara miongoni mwa jamii wengi wakipoteza macho yao.

Kauli yake inajiri baada ya kuripotiwa ongezeko la utumizi wa mihadarati nchini.

BY EDITORIAL TEAM