HabariNews

Idara ya usalama eneo bunge la Shimba Hills yawaonya vijana dhidi ya kujihusisha na wizi wa mifugo.

Idara ya usalama eneo bunge la Shimba Hills yawaonya vijana dhidi ya kujihusisha na wizi wa mifugo na kuuza nyama kuwa atakaye patikana hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.

Akizungumza katika wadi ya Mkongani naibu wa kaunti kamishna eneo bunge hilo, Moses Karwigi amewataka wakaazi kukoma kuendeleza tabia hiyo kwa kisingizio cha hali ngumu ya maisha hali aliyoitaka kuhatarisha usalama wa eneo hilo.

Aidha kamishna huyo amesema kuwa afisi yake imenakili visa kadhaa vya uizi wa mifugo kutoka eneo bunge hilo jambo alilolitaja kutatiza usalama kwa ujumla.

Afisaa huyo amewashauri wakaazi kujihusisha na kilimo kama njia ya kujitafutia riziki badala ya kushiriki wizi wa mifugo ambao unawarudisha nyuma kiuchumi.

BY EDITORIAL DESK