HabariNews

Shirika la kijamii la Hijaby Mentorship Program limeanzisha mradi wa kuihamasisha jamii kuhusu maswala ya usawa wa jinsia kupitia michezo.

Shirika la kijamii la Hijaby Mentorship Program limeanzisha mradi wa kuihamasisha jamii kuhusu maswala ya usawa wa jinsia kupitia michezo.

Mwanzilishi wa shirika hilo Nima Zani amesema kuwa mradi huo unawashirikisha wanawake wa kati ya umri wa miaka 25 hadi 60 katika mchezo wa mpira.

Akizungumza huko mjini Kwale, Zani amedokeza kwamba mradi huo unalenga kuondoa mila potofu zinazochangia wanawake kutengwa katika jamii.

Kwa upande wake kocha wa timu ya Ziwani Women FC Mwanajuma Bedengo amesema kuwa akina mama wengi wamejitokeza kucheza mpira.

Bedengo amelipongeza shirika hilo kwa kuanzisha mradi huo unaolenga pia kukabiliana na visa vya dhulma za wanawake.

BY EDITORIAL TEAM