HabariNews

Waziri Eliud Owalo Athibitisha Kudukuliwa Kwa Wavuti wa E-Citizen

Huduma za serikali kupitia tovuti ya E-Citizen zimerekibishwa na kurejeshwa baada ya huduma hizo kukosekana kwa muda.

Waziri wa habari na mawasiliano Eliud Owalo amethibitisha kudukuliwa kwa huduma hizo.

Aidha huduma za M-pesa, My Safaricom App, M-Shwari, KCB M-pesa, na huduma za kutoa pesa Kutoka benki hadi M-pesa zimerejea kwa sasa.

Licha ya udukuzi huo , Owalo ametoa hakikisho  kuwa hakuna data yoyote iliyoweza kufikiwa na wadukuzi na iliyopotea.

Waziri huyo ameongeza kuwa matukio kama hayo kamwe hayatayumbisha mikakati yao ya kuboresha huduma za kiserikali kwa kupitia mfumo wa kidigitali.

BY EDITORIAL DESK